CENTER
Tuesday, May 30, 2017
NJIA ANAZOTUMIA MUNGU KUKUJIBU MAOMBI
i. Njozi. Dan2:27.
Ii. Ndoto. Mwa 37:1-9.
Iii. Maono. Ezek 8:1-3.
Iv. Ufunuo. Uf 1:1-11.
Tuesday, March 14, 2017
HAYA NDIO MATUKIO YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA PENTECOSTAL CHRISTIAN CENTER - MISUNA SINGIDA
HAPA WAIMBISHA SIFA WAKIJIANDAA KUIMBISHA KATIKA KIPINDI CHA SIFA
MWIMBAJI WA BINAFSI AKIREKEBISHA VYOMBO KATIKA KIPINDI CHA SIFA
WAUMINI WAKICHEZA KATIKA IBADA HIYO ILIFANYIKA SIKU YA JUMAPILI.
WAMAMA WAKIWA NDANI YA YESU WAKIIMBISHA KIPINDI CHA SIFA
WAUMINI WAKIWA WANASIFU NA KUCHEZA SIKU YA JUMAPILI.
KWA YESU KUNA RAHA JAMANI...........
Wednesday, March 8, 2017
NDOTO UNAYOOTA USIKU USIDHARAU FUATILIA UJUE INAMAANA GANI.
MWINJILISTI: LAURENT ELIAS, KANISA LA PENTECOSTAL CHRISTIAN CENTER - MISUNA SINGIDA. |
Kwenye Biblia kuna watu wengi waliota ndoto na tukiziangalia karibu zote zina uhusiano na Mungu.
Kwa mfano ndoto ya kwanza kabisa kwenye Biblia inapatikana kwenye kitabu cha mwanzo 20:1_7,
Hapa tunamuona mwotaji Abimaleki Mfalme wa Gerari, anatokewa na Mungu kwenye ndoto kumuonya amwache Sarah, aliyekuwa amemchukua ili awe mke wake bila kujua kuwa alikuwa mke wa mtumishi wa Mungu Abrahamu.
Huyu Mfalme Abimaleki ni mpagani wala sio mcha Mungu, lakini bado aliota anazungumza na Mungu!
Ndoto nyingine ni ya Yusufu aliota akiwa na miaka 17 akaonyeshwa maisha yake yatakavyo kuwa baadaye,na yote aliyo ota yakaja kutimia baada ya miaka 13,pamoja na kwamba alipitia changamoto nyingi sana.Ali hukumiwa kufa na kaka zake kwa sababu ya ndoto zake ,
Kaka zake wakatafuta njia ya namna ya kumua , wakaona sio vizuri wao wamuue bali wa muuze ili akafie mbali ili ndoto zake zisitimie,Yusuf akauzwa kwa Waishumael ambao wakamleta mpaka MISRI alikouzwa kwenye nyumba ya mfalme akiwa nyumbani mwa Potifah mke wa mfalme alitaka kumbaka japo ni tukio la kipekee mwanamke kutaka kumbaka kijana,lakini kijana Yusufu alikuwa mwaminifu kwa Mungu wake YEHOVA aliyemuonyesha maisha yake yajayo ,akakataa akisema siwezi kumtenda MUNGU dhambi kubwa namna hii.
Tukio hilo la kukataa kutenda dhambi lilimpelekea Yusufu kuingia kwenye changamoto ya tatu kwa kutiwa gerezani
Changamoto ya nne ni pale Yusufu aliposahauliwa na mnyweshaji wa mfalme,alimwahidi baada ya kutafsiriwa ndoto yake akasema sitakusahau nikifika kwa mfalme.
Ndugu yangu Mungu akikupa ndoto uwe tayari kukabiliana na changamoto nyingi kabla ndoto yako haijatimia.
Ndoto nyingine ni za wahudumu wa mfalmeFarao. Mwanzo 40:1- wote wawili walitenda kosa moja,walihukumiwa pamoja,waliwekwa gereza moja wote wawili,waliota ndoto zenye jumbe zinazoelekeana na kazi zao kwa mfalme ,ndoto ya mmoja ilikuwa njema naya mwingine ilikuwa mbaya.
Hapa tunajifunza mgawanyo wa ndoto kuwa kuna ndoto mbaya, na kuna ndoto nzuri.
Mwota ndo mwingine ni mfalme Farao., Mwanzo 41:1- huyu tena alikuwa siyo mcha Mungu ndiyo maana hata alipoota ndoto aliwaita waganga na wachawi ili wamtafsirie ndoto yake, japo pia aliota ndoto ilotoka kwa Mungu ,na hii ndiyo ndoto iliyotimiza na kudhihirisha ndoto aliyoota Yusufu miaka 13 iliyopita.
Ukiziangalia ndoto zote hizi unaziona zina ujumbe wa Mungu moja kwa moja,na kila ndoto kwenye Biblia ilikuwa ya kweli na ikatimia sawasawa na ilivyootwa.
Ndugu zangu tukisoma kwenye Biblia tunaona nabii Yoeli alionyeshwa juu ya kizazi chetu kuota ndoto.
YOELI 2:28. Hata itakuwa baada ya hayo ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwil, wana wenu waume kwa wake watatabiri, wazee wenu wataota ndoto na vijana wenu wataona maono.
Hapo Yoeli anaona wana wa kike na wa kiume wanatabiri,wazee wanaota ndoto na vijana wanaona maono.Tunaweza kujiuliza je unabii wa Yoeli umeshaanza kutenda kazi? Jibu ni ndiyo .
Matendo2:16-17; lakini jambo ni lile lililonenwa kwa kinywa cha Nabii Yoeli, itakuwa siku za mwisho asema Mungu nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabir, na vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto!
Kupitia maelezo hayo ya Petro akithibitisha kutimia kwa unabii wa Yoeli, tunapata picha niwazi aliyotabiri Yoeli yanatendeka sasa katika kizazi chetu .Lakini pia kuna jambo la ajabu linaloaendelea duniani leo, Yoeli alitabiri ndoto zitaotwa na ‘mtu amelala anaota anajamiahiana na mtu asiye mke wake au mume wake, mara mtu anaota anakabwa na JINAMIZI! Mara mtu anaota anakula manyama ya ajabu ajabu au vyakula, Ndoto za siku hizi nyingi zimejaa vitisho mtu anamka amekata tamaa kabisa au kavunjika moyo kabisa kwasababu tu ya ndoto alizo ota, ndoto nyingi siku siku hizi zimebeba jumbe za hatari kuliko kuleta matumaini. SASA TUJIULIZE JE!!? Hizi ndoto za kuota mara unakabwa,mara unaota unafukuzwa na kambako jeusi je hizi ndizo ndoto alizoziona Yoeli?.
wazee baada ya MUNGU kumimina ROHO wake .Lakini kinyume chake siku hizi kila mtu anaota ndoto,kuanzia watoto wadogo mpaka wazee,na ndoto zenyewe ziko tofauti kabisa na zile ndoto tulizoziona kwenye Biblia ambazo zilikuwa na ujumbe wa MUNGU,bali za sasa ni za ajabu:
ZEKARIA 10:2
‘’Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili ,nao waaguzi wamenena uongo;nao wameleta habari za ndoto za uongo,wafariji bure;kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo ,wateswa,kwa sababu hapana mchungaji.’’
Kupitia Zekaria tunaweza kuona chanzo cha ndoto za sasa ni kupitia vinyago (ibada ya sanamu, na mawakala wa shetani waaguzi)
KUNA SABABU KUU MBILI ZA MAWAKALA WA SHETANI KULETA NDOTO ZA UONGO:
(a) Kuwanajisi watu ili wapate kuwatesa.
(b) Kwa sababu hapana mchungaji sawasawa na zekaria alivyosema
Hii inamanisha kuwa kanisa limelala,watu wanakwenda kanisani kwa ajili ya kuimba tenzi na pambio, Jambo hilo siyo baya,lakini wachungaji tujue kanisa lipo kwa ajili ya kupambana na malango ya kuzimu. MATHAYO 16:18; Namii nakwambia leo wewe ndiwe Petro na juu ya Mwamba huu nitalijenga kanisa lango wala milango ya kuzimu haitakishinda. Na kwa kuthibitisha kuwa kanisa lijijue kuwa lipo vitani wakati wote,Mtume P AULO anaeleza aina ya vita vyetu katika .Waefeso 6:12; kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Napenda utambue kuwa tunapo jifunza habari za ndoto tunaongelea mambo ya rohoni . mwanadamu ameganyika vipande viwili mtu wa ndani (Inner man) na mtu wa nje yaani mwili (outer man) tusemeje sasa mwanadamu ninani? Mwanadumu ni roho yenye nafsi inayokaa ndani ya nyumba na hiyo nyumba inaitwa mwili. 2Korintho 12:2 Namjua mtu mmoja katika Kristo yapata sasa miaka kumi na minne (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa mpaka mbingu ya tatu.
Hapa Paulo anajaribu kukumbuka miaka kumi na nne iliyopita siku alipotokewa na Bwana Yesu. Lakini pia kupitia Mtume Paulo tunathibitisha kuwa mtu anaweza kuwa ndani ya mwili na nje ya mwili. Jambo hutokea kwenye ndoto pia mtu amelala Moshi lakini anaweza kuota yuko Nairobi na akaona vitu vingi napengine nayeye akashiriki kwa namna moja au nyingine lakini mwisho wa siku anamka na ndipo anatambua kwamba kumbe ni ndoto tu! Sasa huko kwenye ulimwengu wa roho kwakuwa tumeona mtume Paulo akisema kuna Falme na mamlaka, wakuu wa giza na majeshi ya pepo wa baya hao ndiyo wanavuvia ndoto mbaya Duniani. Kwa watu walio na Yesu(waliokoka) ukitaka kuwa salama na kujitenganisha na ndoto mbaya nilazima uchukue hatua ya kuwasambaratisha hawa maadui kwenye ulimwengu wa roho kwa kutumia jina la YESU!
Huu siyo wakati wa kulia lia na kulalamika,huu ni wakati wa kuvaa silaha za MUNGU tayari kwa kumsambaratisha shetani na mawakala zake wanaotuletea ndoto za ajabu ajabu,na pia tunayo damu ya YESU iliyomwagika msalabani kwa ajili yetu.
SASA: Tuitumie damu hii kufuta ndoto zote za kishetani tulizoota, tunazozikumbuka na tusizo zikumbuka,tuzifute ndoto zote mbaya kwa damu ya mwanakondoo YESU KRISTO.
Tuesday, March 7, 2017
Swali: "Je, Yesu ni Mungu?
Swali: "Je, Yesu ni Mungu? Je, Yesu alitoa madai ya kuwa yeye ni Mungu?"
Jibu: Yesu hakunakiliwa mahali popote katika biblia akisema, “Mimi ni Mungu.” Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba hakusema kuwa yeye ni Mungu. Kwa mfano ni maneno ya Yesu katika Yohana 10:30, “ Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa kwanza, hili linaweza kuwa si dai la kuwa Mungu. Lakini angalia mapokezi ya ujumbe huu kwa wayahudi, “hatukupigi mawe kwa lengine lile ila kufuru, kwa sababu wewe ni mwanadamu, unayejidai kuwa Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa matamshi ya Yesu kuwa alijijulisha kwao kuwa yeye ni Mungu. Katika aya zifuatazo hawasahihishi wayahudi kwa kusema, “si kusema mimi ni Mungu.” Hii ina maana ya kuwa aliposema haya yafuatayo alikuwa akimaanisha kweli kuwa ni Mungu, “Mimi na Baba yangu ni mmoja” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwingine. Yesu akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena kwa ajili ya hayo wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Je, wayahudi wangetaka kumpiga mawe yesu kama haingekuwa ya kuwa alisikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?
Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!
Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1). Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.”
Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.
Sababu muhimu ya kwamba Yesu sharti awe Mungu ni kwamba kama si Mungu, kufa kwake hakungetoshea kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu pekee ndiye angeweza kulipia adhabu kama hiyo. Mungu pekee ndiye angeweza kufidia dhambi za ulimwengu wote w (Wakorintho wa pili 5: 21), afe na afufuke kuthibitisha ushindi juu ya dhambi na mauti.
Monday, March 6, 2017
MAOMBI NI NINI?
Math 7:7 "Ombeni,nanyi mtapewa,tafuteni nanyi mtaona,bisheni nanyi mtafunguliwa"
1.Maombi ni kutafuta,kubisha hodi kwa Mungu.Luka 18:1 "Akawaambia mfano,ya kwamba imewapasa kumwomba MUNGU sikuzote wala wasikatetamaa"
2.Maombi ni kumwendea MUNGU
Ebr 11:6b "Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko,na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao"
3.Maombi ni kuzungumza na Mungu Isaya 1:18 "Haya njoni tusemezane,asema bwana wa majeshi,
1.Maombi ni kutafuta,kubisha hodi kwa Mungu.Luka 18:1 "Akawaambia mfano,ya kwamba imewapasa kumwomba MUNGU sikuzote wala wasikatetamaa"
2.Maombi ni kumwendea MUNGU
Ebr 11:6b "Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko,na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao"
3.Maombi ni kuzungumza na Mungu Isaya 1:18 "Haya njoni tusemezane,asema bwana wa majeshi,
4.Maombi ni kuweka wazi haja/mahitaji yetu mbele za MUNGU ,filip 4:6 "Msijisumbue kwa Neno lolote,bali katika kila Neno kwa kusali na kuomba,pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu"
5.Maombi ni Ibada mbele za MUNGU..MDO 13:2 "Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga,ROHO MTAKATIFU akasema,
6.Maombi ni kupigana vita vya kiroho,EFESO 6:18 "Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho,mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu"
7.Maombi ni kutulia na MUNGU Isaya 30:15 "kwa maana Bwana MUNGU asema hivi,kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa,nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kumtumaini lakini hamkukubali"
KWANINI YATUPASA KUOMBA?? MATH 7.7
1..Tunaomba ili tupewe haja zetu, "Ombeni nanyi mtapewa",Tena neno la MUNGU linasema wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi,Yakobo 4:2 "Mwatamani wala hamna kitu,mwaua na kuona wivu,wala hamwezi kupata,mwafanya vita na kupigana,wala hamna kitu kwa kuwa HAMWOMBI"
2.Ni agizo kutoka kwa YESU..Luka 18:1 "Akawaambia mfano,ya kwamba imewapasa kumwomba MUNGU siku zote,wala wasikate tamaa"
1THES 5:17 "Ombeni bila kukoma"
3.kwa sababu kuomba ni Huduma..huponya taifa,familia,kanisa na watu wanaponywa magonjwa na shida zao na kazi yake Jehova hufanikiwa
2NYAK 7:14 "Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu,watajinyenyekesha,na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao"
4. Isaya 59:16 "Akaona ya kuwa hapana mtu,akastaajabu kwa kuwa hapana MWOMBEZI basi mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu na haki yake ndiyo iliyomsaidia"
Yak 5:14-16 "Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa nao wamwombee na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi,na kuombeana mpate kuponywa,kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii"
5..Kwa sababu ya kujenga mahusiano yetu karibu na Mungu
YAK 4:8 "Mkaribieni Mungu naye atawakaribia ninyi,itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu,enye wenye nia Mbili"
6..Kwa kuwa MUNGU ni Baba na sisi ni watoto wake,yatupasa kumwomba haki zetu tukiwa kama watoto..
MATH 6:9 "Basi ninyi salini hivi,Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe,ufalme wako uje"
5.Maombi ni Ibada mbele za MUNGU..MDO 13:2 "Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga,ROHO MTAKATIFU akasema,
6.Maombi ni kupigana vita vya kiroho,EFESO 6:18 "Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho,mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu"
7.Maombi ni kutulia na MUNGU Isaya 30:15 "kwa maana Bwana MUNGU asema hivi,kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa,nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kumtumaini lakini hamkukubali"
KWANINI YATUPASA KUOMBA?? MATH 7.7
1..Tunaomba ili tupewe haja zetu, "Ombeni nanyi mtapewa",Tena neno la MUNGU linasema wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi,Yakobo 4:2 "Mwatamani wala hamna kitu,mwaua na kuona wivu,wala hamwezi kupata,mwafanya vita na kupigana,wala hamna kitu kwa kuwa HAMWOMBI"
2.Ni agizo kutoka kwa YESU..Luka 18:1 "Akawaambia mfano,ya kwamba imewapasa kumwomba MUNGU siku zote,wala wasikate tamaa"
1THES 5:17 "Ombeni bila kukoma"
3.kwa sababu kuomba ni Huduma..huponya taifa,familia,kanisa na watu wanaponywa magonjwa na shida zao na kazi yake Jehova hufanikiwa
2NYAK 7:14 "Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu,watajinyenyekesha,na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao"
4. Isaya 59:16 "Akaona ya kuwa hapana mtu,akastaajabu kwa kuwa hapana MWOMBEZI basi mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu na haki yake ndiyo iliyomsaidia"
Yak 5:14-16 "Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa nao wamwombee na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi,na kuombeana mpate kuponywa,kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii"
5..Kwa sababu ya kujenga mahusiano yetu karibu na Mungu
YAK 4:8 "Mkaribieni Mungu naye atawakaribia ninyi,itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu,enye wenye nia Mbili"
6..Kwa kuwa MUNGU ni Baba na sisi ni watoto wake,yatupasa kumwomba haki zetu tukiwa kama watoto..
MATH 6:9 "Basi ninyi salini hivi,Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe,ufalme wako uje"
MWINJILIST LAURENT
MUNGU AKUBARIKI
KWA MAOMBEZI YA KUFUNGULIWA FIKA KANISANI SASA.
AU PIGA SIMU: 0763652896, 0782859946,0714890889--mchungaji Laurent Mpoma
Subscribe to:
Posts (Atom)